Wapendwa wanablog! Wazoefu na wale tunaoanza, natumaini mtakuwa mmeupokea ujio wangu. Hakika ni mgeni lakini najua kwa nguvu zenu kila mmoja kwa moyo wa dhati tutazidi kutiana nguvu na sisi tulio wachanga tutakua na kufikia ujana,utu-uzima na hata kuwa wazee wa kublog. nafurahi kuwa nimefikia hatua hii ya kuwa bloger,nina mengi ambayo nitachangia na kuendeleza hii fani ya kupeana nyuzi mtandaoni. Nitafurahi sana kupokewa vema na klabu za kublog ili tuweze kuimarishana na kudumishana katika fani hii.
Kwa leo ninaomba tu niwajulishe kuwa nimeingia ulingono na ninatarajia kupata mapokezi yenu ili niweze kupata nguvu zaidi na zaidi za kuendelea. Asanteni sana!
Wednesday, April 19, 2006
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
4 comments:
Karibu sana ndugu yetu. Tupo pamoja katika kujenga jumuiya yetu hii. Tunatarajia mengi toka kwako.
Asante sana bwana Ndesanjo kwa kunikaribisha. Nimekutembelea na kuona nitapata mengi sana kutoka kwenye blog yako. Ninasema hivyo kwa vile kwa haraka haraka nimeona una mambo mengi sana ambayo mpaka niyaone yote itakuwa ni balaa! Nilidhani ni magazetini tu kumbe sivyo. Najihisi unanishika mkono nisianguke! Asante sana!
Karibu! Karibu mpaka ndani. Mbali na mema tunayoyatarajia kutoka kwako kama alivyosema Ndesanjo, mie pia natarajia samaki kutoka ziwa Vicky
Karibu sana. Kama we ni mwanamamzingira basi karibia www.jadili.blogspot.com
Post a Comment